Tarehe ya kufunga 01/12/2024
Background
Electronic media (M-Net), kitengo cha maudhui cha MultiChoice Group, kimeendelea kuwapatia watazamaji burudani ya hali ya juu zaidi kwa njia ya video kwa zaidi ya miaka 30. Chaneli za M-Net zinatoa maudhui ya kuvutia na kusisimua, zilizosheheni vipindi halisi vya Kiafrika pamoja na filamu na tamthilia bora za kimataifa. Tunajitahidi kila mara kukuza tasnia ya filamu kwa kuendeleza vipaji vya watayarishaji na wahusika kwa viwango vya kimataifa.
Maisha Magic Bongo ni chaneli ya burudani inayopatikana kwenye DStv kupitia chaneli 160, chini ya M-Net. Tumejikita katika kutoa maudhui yanaolezea uhalisia wa maisha ya Kitanzania, kwa kuzingatia mpangilio wa kijamii na kifamilia.
Lugha inayotumika kwa kiasi kikubwa ni Kiswahili, na lugha ya Kingereza kwa kiasi kidogo.
Muhtasari: Kile Tunachotafuta
Maisha Magic Bongo inatoa fursa kwa kupokea mapendekezo ya vipindi ya vyenye uhalisia (Reality Show) kutoka kwa watayarishaji wa Kitanzania. Kipindi kinapaswa kuwa cha kusisimua, chenye kuvutia watu wa rika zote, huku kikiibua mijadala na kujenga wafuasi.
Zinahitajika episode 25 kila moja iwe na dakika 45.
KICHWA CHA MUHTASARI: Kipindi cha Uhalisia (Reality Show)
PLATTFORM: Maisha Magic Bongo
GENRE: Uhalisia
HADHIRA LENGWA: Umri kuanzia 16 – 45
MFULULIZO: 25Eps x 45 min
LUGHA: Swahili
Editorial Guide:
Mawazo yanapaswa kuwa halisi, ya kujenga na ya kuvutia, uhalisia huu lazima uwe na mandhari ya kuwashika na kuwavutia watazmaji. Wahusika lazima wawe mtu/watu wanaojulikana wenye ufuasi na ushawishi katika jamnii zetu.
Yanayohitajika katika Pendekezo lako
Kanuni za mawasilisho
Mawasilisho yote lazima yawasilishwe kwenye mfumo wa Power Point presentation, yenye kurasa zisizo zidi 15 kupitia.
HAYATAKUBALIKA
Ufundi na ufanisi unaozingatiwa na Maisha Magic Bongo utatolewa katika makubaliano ya uaandaji.
N.B: Usipofanikisha kuambataisha nyaraka zote tajwa hapo juu,pendekezo lako halitapokelewa.
Mchakato wa Uteuzi:
Taratibu zetu za uchaguzi zitachukua takriban wiki nane
Ikiwa hautapata ujumbe wowote kutoka kwetu ndani ya siku 90 baada ya kuwasilisha pendekezo lako, ujue kwamba haukufanikiwa