Maisha Magic Bongo, chaneli nambari 160 ndani ya DStv, ni chaneli inayodumisha utamaduni wa Mtanzania kupitia burudani. Kama chaneli ya burudani ya saa 24, inatoa ladha mbalimbali kwa soko kubwa la Watanzania kwa mchanganyiko mzuri wa vipindi vya maisha na maudhui asilia ya ndani.
Ikizingatia uhalisia, chaneli hii inawasilisha thamthilia, telenovela, muziki, vipindi vya uhalisia, vipindi vya ucheshi na zaidi vilivyotengenezwa kwa Kiswahili, kuhakikisha kwamba hadithi zinawagusa watazamaji wa ndani.
Maisha Magic Bongo si chaneli tu; ni jukwaa linaloendeleza na kusaidia sekta ya sanaa na ubunifu Tanzania, pia kuwapa burudani na kuwaelimisha watazamaji.
Chaneli Yetu:
Maisha Magic Bongo – DStv Chaneli 160
Kituo hiki kwa sasa hakipokei maombi yoyote.