Tanzanian Movies

Closing date 31/12/2022

Maisha Magic Movies Commissioning Brief (Swahili)

M-Net, tawi moja wapo la kampuni ya MultiChoice, imekuwa kinara katika kuwaletea watazamaji burudani ya hali ya juu kwa zaidi ya miaka 30. Chaneli za M-Net zimekuwa kivutio cha maudhui ya burudani za kusisimua zikijumuisha sinema na tamthilia za asili ya Kiafrika na zile za kimataifa. Tunaendeleza dhamira yetu pana ya kukuza tasnia ya filamu kwa kuinua na kujenga vipaji vya wazalishaji na hivyo kusaidia kuinua vipaji vya ndani na vya kimataifa.

Uandaaji wa maudhui

MNet ingependa kufadhili filamu halisi za kitanzania zinazolenga mila na desturi za kitanzania, mapenzi, mahusiano na maisha ya watu mbalimbali ya kila siku.

Filamu inatakiwa kuwa katika lugha ya Kiingereza au Kiswahili na kutafsiriwa kwa lugha ya kiingereza (subtitle). Simulizi inatakiwa kuwa yakusisimua na kumfanya mtazamaji kuwa na hamu na shauku ya kusubiria filamu zingine.

Mahitaji yanayopendekezwa

·        Muda- Dakika 90

·        Lugha -Kiswahili

·        Mwongozo wa filamu

·        Wasanii watakaocheza

·        Majina kamili ya timu ya waandaaji

·        Bajeti ya Awali

·        Demo ya kazi yoyote ya awali ya muombaji

·        Stakabadhi ya kimkataba, ikielezea majina kamili ya kampuni, waongozaji na wadau, vielelezo vya usajili wa kampuni, hati za usajili za VAT na anuani kamili.

 

Tathmini

·        Risiti za mapendekezo zitatambulika kwa njia ya barua pepe.

·        Viwango vya kitaalam na uhariri vinavyotakiwa na MNet vitawekwa kwenye mkataba wa makubaliano.

·        MNet ndio watafanya uhariri wa mwisho na udhibiti wa ubunifu kulingana na matarajio ya filamu inayotakiwa.

Submit an Idea