Commissioning Brief - Movie Channel Tanzania

Tarehe ya kufunga 15/03/2021

Uandaaji wa maudhui

MNet ingependa kufadhili filamu halisi za kitanzania zinazolengamila na desturi za kitanzania, mapenzi, mahusiano na maisha ya watu mbalimbali ya kila siku.

Filamu inatakiwa kuwa katika lugha ya Kiingereza au Kiswahili na kutafsiriwa kwa lugha ya kiingereza (subtitle). Simulizi inatakiwa kuwa yakusisimua na kumfanya mtazamaji kuwa na hamu na shauku ya kusubiria filamu zingine.

Mahitaji yanayopendekezwa

 • Kulenga watu wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45
 • Muda- Dakika 90
 • Lugha -Kiswahili au Kiingereza
 • Mwongozo wa filamu
 • Wasanii watakaocheza
 • Majina kamili ya timu ya waandaaji
 • Bajeti ya Awali
 • Demo ya kazi yoyote ya awali ya muombaji
 • Stakabadhi ya kimkataba, ikielezea majina kamili ya kampuni, waongozaji na wadau, vielelezo vya usajili wa kampuni, hati za usajili za VAT na anuani kamili.

            Tathmini

 1. Risiti za mapendekezo zitatambulika kwa njia ya barua pepe.
 2. Mapendekezo yatapitiwa na jopo la majaji watakaochaguliwa na Wakuu wa Chaneli ambao watatolea maelezo mafupi mapendekezo yaliyopitishwa.
 3. Kuchagua mapendekezo yaliyoshinda.

Mawasilisho

Ukusanyaji wa mapendekezo itakuwa hadi tarehe 14 Machi 2021 kupitia tovuti yetu ya https://submissions.mnetcorporate.co.za/channel/maisha-magic-bongo

 Mwisho wa Ukusanyaji: 15/03/2021

 • Viwango vya kitaalam na uhariri vinavyotakiwa na MNet vitawekwa kwenye mkataba wa makubaliano.
 • MNet ndio watafanya uhariri wa mwisho na udhibiti wa ubunifu kulingana na matarajio ya filamu inayotakiwa.

Mawasilisho yote yatumwe kwenye tovuti yetu

https://submissions.mnetcorporate.co.za/channel/maisha-magic-bongo

Submit an Idea